TAREHE YA MKUTANO
Mkutano utafanyika tar. 2/03/2013 siku ya Jumamosi
ENEO LA MKUTANO
Mkutano utafanyika mjini Matamba, ukumbi utatangazwa baadaye
NAMNA YA KUFIKA (kwa wenzetu ambao hawajafika Matamba siku nyingi ni lazima tuwakumbushe namna ya kufika Matamba).
Kufika mkutanoni ni rahisi
sana kwani kokote utakakotokea utashuka Chimala na kuna magari mengi
sana ya kupandisha milimani, na kama bahati mbaya ukichelewa unaweza
kuwasiliana na mratibu gari iliyopo Chimala ikakusubiria, Ikumbukwe ni
mkutano wa Wawanji hivyo kuna ushirikiano wa hali ya juu.
Kama una usafiri binafsi,
kwa kuwa ni kipindi cha mvua ukifika Chimala unaweza kuchagua njia ya
kupita au Mfumbi au Ngoje kutokana na aina ya gari utakayokuwa umesafiri
nayo, lakini njia kwa kiwango fulani zinapitika.
WASILIANA NA MRATIBU WA MKUTANO
Namba ya simu ya mratibu wa mkutano ni +255 753900488, Tafadhali wasiliana naye kama utakuwa na swali ambalo halijibiwi na maelezo yaliyotolewa hapa.
MALAZI
Kwa kweli tunamshukuru sana Mungu kwani Matamba pana hoteli nzuri mpaka za kitalii
na kama hujisikiii kulala hotelini Wawanji ni wakarimu sana utapata
huduma ya malazi na chakula kutokana na utaratibu ambao viongozi wa
mkutano watauandaa.
CHAKULA
Chakula cha mchana siku ya
mkutano kitatolewa, ndiyo maana tunawasisitiza wawanji kuhudhuria na
kuchangia angalau Tsh.5000 kwa ajili ya vinywaji laini na chakula cha
mchana. kama hutaweza kuhudhuria unaweza kutuma mchango wako kwa M-pesa
kwa namba hizi. 0756-286018
TAFADHALI FIKA BILA KUKOSA KWA MAENDELEO YA UWANJI
Maelezo Mengine (kama ajenda za mkutano n.k) yatatolewa baadaye
No comments:
Post a Comment