Our Activities and Projects/Shuguli na Miradi ya UDT

Uwanji Development Trust (U.D.T) is a charitable, non-profit making, community-based trust. UDT was established in 2008 and became registered on 28th July 2010 by a certificate of registration no.S.A.16950 under society ordinance act 1954, society Act cap 337 (R.E.2002) of the United Republic of Tanzania. UDT is involved with several activities which include, but are not limited to, the following; 1.Promoting access and provision of quality education; 2. Provide assistance on health matters with special focus on HIV/AIDS; 3.Take measurable actions on the protection of environment; 4. Cooperate with governmental and non governmental stakeholders for technical and financial sustainable development issues and act as implementing agency; 5. Perform any other activity for the sustainable development of Uwanji people.
Join our cause by writing us: Our email address is udt2010[at]live.com or contact one of the following for more details; Chaiperson -Toba Nguvila - +255 755 097181. Deputy Chairperson - Rev. Naibu Nyambo +255 754 387364. Secretary - Valentine Malila - +255 755 474579. Deputy Secretary - Amani Mbwilo - +255 753 858527.

20 Aug 2013

NDEGE AITWAYE KWALE AWEZA KUWA CHANZO CHA KIPATO CHA UHAKIKA!

[Habari hii imenukuliwa kutoka www.wavuti.com]

Kuna wakati nilijiamini kuwa ninakifahamu vilivyo Kiswahili. Lakini kadiri siku zinavyokwenda, ndiyo ninavyozidi kugundua kuwa nina uhaba wa misamiati ya lugha yangu Mama.

Kwa mfano, kwetu tukiwa watoto tulikuwa tukimwinda ndege/kuku huyu nyakati za masika na tulimtambua kwa jina la 'kware,' sikufahamu kuwa jina lake jingine ni 'tombo' mpaka nilipoisoma habari ifuatayo...
Picture
Madai kwamba ulaji wa bidhaa za tombo husaidia afya ya mtu ni sehemu ya sababu ya hivi karibuni ya kuongezeka kwa mahitaji nchini Kenya. [Bosire Boniface/Sabahi]
Kutokana na hali ya wimbi kubwa la mahitaji ya bidhaa za tombo katika miezi ya hivi karibuni kumelazimisha wafanyabiashara nchini Kenya kote kujiingiza katika biashara mpya ya ufugaji wa tombo.

Mkaazi wa Kiambu Andrew Githinji aliiambia Sabahi kwamba ufugaji wa tombo hauna gharama kuendesha na unaleta mapato mazuri: "Hauhitaji eneo kubwa. Tofauti na kuku ambao wanahitaji eneo kubwa, viota vya [tombo] vinaweza kuwekwa vibarazani," Githinji alisema.

Alisema kwa mara ya kwanza alivutiwa na mradi kama huo baada ya kusoma kwenye orodha ya vyakula katika hoteli yenye nyota tano huko Nairobi mwezi Januari 2012.

Alipata kuona kitu ambacho hakuwa anakijua: nyama ya tombo ya kubanika. "Nilifikiri kuwa tombo alikuwa aina ya chakula kinachotoka baharini, katika kuchunguza, nilimuuliza mhudumu na alisema ilikuwa ni ndege," Githinji mwenye umri wa miaka 33 alisema.

Githinji, ambaye pia anafuga sungura, alianza kufanya utafiti kuhusu tombo na kugundua kuwa watu wanamfuga ndege huyo: "Sikuwa najua kuwa ndege huyu, ambao wanapatikana kwa wingi kijijini kwangu, angeweza kufugika," alisema.

Alinunua ndege wake 20 kwa mara ya kwanza kwa shilingi 250 kila mmoja (dola 2.85), Githinji alisema, akiongezea kwamba kwa sasa ana tombo 520: "Cha kusikitisha tu ni kwamba niligundua biashara hii kwa
kuchelewa," alisema Githinji. "Lakini nitwafikia wengine na kwa muda wa miaka miwili nitakuwa na mashine yangu ya kutotolesha itakayosaidia kutotoleshea vifaranga."

Mkaazi wa Mombasa Alex Mureithi, mwenye umri wa miaka 39, alisema alishangazwa kwenda katika shamba la tombo baada ya kutembelea katika duka la jumla mwezi Julai 2012.

Aliona dazeni za "mayai tofauti ya tombo" katika rafu ambalo alidhania ni nakshi ya jiwe la sabuni na kugundua kwamba walikuwa wakiuza kwa shilingi 650 (dola 7.43) ukilinganisha na trei la mayai 30 kwa bei ya shilingi 400 (dola 4.57).

Mureithi kisha alizungumza na meneja wa duka ambaye alimwambia kwamba wafugaji wa tombo hawawezi kutosheleza mahitaji ya soko, ingawa tombo hutaga mayai karibia kila siku: "Nilitambua kuwa yalikuwa ni matembezi yenye faida hivyo nilinunua ndege 10. Sasa ninao 900," Mureithi aliiambia Sabahi. "Sijui nini kitatokea katika ufugajii wa tombo kwa siku zijazo lakini sasa ninavuna faida ya juu kabisa. Anaziuzia hoteli nne huko Mombasa na Nairobi, ambazo zinatoa agizo kwa kila mwezi kwa wafugaji kupata mayai na nyama ya tombo", alisema.

Anatoza mayai yake kwa shilingi hadi 60 (senti 68) kwa kila moja na tombo mzima kwa shilingi 800 (dola 9.14).

Mureithi pia anawafundisha na kuwatembeza wanaotaka kuwa wafugaji wa tombo katika shamba lake kwa kuwatoza shilingi 3,000 (dola 34.3), alisema.

Nzuri kwa afya ya kila mtu? Mahitaji ya mayai na nyama ya tombo yamesababishwa na ripoti ambazo zinaeleza kwamba kula tombo una thamani ya kiafya.

Yunuke Nyanchama, mkaazi wa Kisii mwenye umri wa miaka 67, aliiambia Sabahi kwamba amekuwa akila mayai ya kituitui kwa miaka miwili iliyopita. Alipatikana na kisukari mwaka 2004 na amekuwa akitumia dawa nyingi bila kuwa na mabadiliko mazuri.

Wakati wa ukaguzi wa kawaida mwezi Mei 2011, hata hivyo daktari wake alipendekeza kwamba ajaribu mayai ya tombo:"Nilistaajabishwa na tiba hiyo, lakini baada ya kutumia mayai hayo na nyama ya ndege, kuna mabadiliko makubwa," alisema.

Vincent Juma, daktari wa Hospitali ya Wilaya ya Mbagathi, aliiambia Sabahi kwamba wakati kulikuwa hakuna utafiti kuhusu faida za kitabibu za mayai na nyama ya tombo, watu wengi wamethibitisha kuwa unafuu baada ya kuvitumia: "Miongoni mwa wagonjwa ambao walirekodiwa [ni] wale waliopata unafuu mkubwa [ni] wale waliokuwa wakisumbuliwa na kifua kukuu na vidonda. Mgonjwa wa saratani alisema kwamba maumivu aliyokua nayo yamepungua baada ya kutumia mayai hayo," Juma alisema

Wafugaji wa tombo wanahitaji leseni Kwa sababu tombo wanachukuliwa kama wanyamapori, wafugaji wa tombo kwanza wanahitaji kuomba kibali kutoka katika Huduma za Wanyamapori Kenya (KWS), msemaji wa shirika hilo Paul Udoto aliiambia Sabahi.

Kabla ya huduma hiyo kutoa leseni, viongozi wa KWS wanapaswa kukagua shamba lake kuhakikisha kwamba linakidhi mahitaji kwa ajili ya kufuga tombo, alisema Udoto.

Malipo ya mwaka kwa ajili ya leseni yanagharimu hadi shilingi 2,000 (dola 22.9), alisema, akiongeza kwamba kibali kinaweza kuhuishwa kwa mwaka kulingana na kukamilisha baadhi ya masharti, ikiwa ni pamoja na usafi.

KWS inaendesha ufuatiliaji na ukaguzi wa mashamba kwa vipindi, na hufuta leseni kutoka kwa wafugaji ambao wanakiuka masharti hayo, alisema Udoto

Huduma hiyo ina maombi mengi ya kibali kutoka kwa watu binafsi na vikundi ambavyo vinataka kufanya ufugaji wa tombo, alisema.

Serikali inahamasisha biashara iliyorekebishwa kama njia ya kuanzisha ajira na kuwapa Wakenya mbadala wa vyanzo vya chakula, alisema Udoto, akiongeza kwamba biashara ya tombo imeota mizizi katika mikoa ya Pwani, Mashariki na Kati pamoja na Kaunti ya Nairobi.

KWS pia inatoa leseni za kufuga wanyamapori wengine kama mamba ili kusaidia katika jitihada za utunzaji, alisema. --- Imeandikwa na Bosire Boniface na kuchapishwa kwenye gazeti la gazeti la Sabahi.

20 May 2013

Usikubali kuwa mnyonge wa kiuchumi ndani ya Tanzania - Meshack Maganga

Makala hii elimishi imeandaliwa na Meshack Maganga, IRINGA.

Kwa muda mrefu nimekuwa nikitoa hamasa kwa vijana wenzangu wa kike na kiume na watu wa kada mbalimbali, wito wangu umekuwa nikuwataka vijana wenzangu kauanza utamaduni wa kuwekeza kwa muda mrefu na kujifunza ujasiriamali. 
Ninaandika kutoa ushuhuda wa niliyoyafanya kwa muda wa miaka miwili iliyopita,na pia ninaandika makala hii kujibu baadhi ya maswali ambayo baadhi ya rafiki zangu wamekuwa wakiniuliza.

Nilianza kujishighulisha na ujasiriamali nilipokuwa chuo kikuu mwaka wa pili, kwa kuuza vocha na  kazi ya ‘steshenari’ na uuzaji wa laptop, sikuendelea nazo sana kwa sababu ya kubanwa na masomo ya chuo.

Nilipomaliza chuo 2010, nilianza kilimo cha mboga na kufuga kuku hapa Iringa mjini, baada ya hapo kaka yangu alianza kunihimiza kuhusu kilimo cha miti ambacho yeye mwenyewe anafanya. Na baadaye nikakutana na rafiki yangu Albert Sanga ambaye pia anajishughulisha sana na kilimo cha miti.

Tangu 2011 nilinunua shamba la ekari 10 na kuzipanda miti hela ambayo niliipata baada ya kuuza matango niliyolima kijijini Kalenga,nikaongeza bidii zaidi ya kulima matango na kununua mashamba,l eo nina ekari nyingi.

Albert sanga, mjasirimali na mwekezaji alipata kuandika haya kuhusu mimi:- “UNASUBIRI UPATE MTAJI? OPSss! UNAWEZA KUFA MASIKINI!

Nina rafiki yangu mpambanaji kweli kweli na msomi wa chuo kikuu wa mambo ya maendeleo na elimu; na mtaalamu 
wa IT, anaitwa Meshack Maganga. Wakati fulani huko nyuma alinifuata na kuniambia, "Sanga nimeamua kuanza kui-invest katika mashamba ya miti; mtaji wa kuanzia nina tsh elfu ishirini na tano, (25,000?/=). Nikamwambia "Kupata ekari moja si chini ya laki sita na wewe una tsh 25,000/= utawezaje?" Akanijibu "Nitaweza!", Sikumwelewa!

Kumbe alikuwa anaona mbali! Alichofanya alichukua hiyo 25,000/= akaenda nayo eneo moja linaitwa Kalenga (km 20 kutoka Iringa mjini) huko akalima matango. Angalia mchanganuo: Shamba nusu eka akakodi kwa tsh 10,000/=, mbegu za matango akanunua Tsh. 7,000/=. Kwenye kulima akalima kwa mikono yake akisaidiana na kibarua mmoja. Fedha iliyobaki 8,000/= akalipa kibarua na kununulia dawa ya kuua wadudu. Alipokuja kuvuna akapata tsh 800,000/= (laki nane).

Alipokuja na fedha hii tukaenda kutafuta shamba la miti akaanza na ekari moja huku pesa nyingine akairudisha shambani. Hivi leo Bw. Maganga ana ekari zisizopungua hamsini za mashamba ya miti na anaendelea na kilimo cha umwagiliaji. Lakini HAPO amefika kwa kutumia tsh 25,000/= tu. Tunaposema hauhitaji mamilioni kujiajiri tunatamani ujifunze kutoka kwa waliofanikiwa kama Bw. Maganga. Unaweza kumwandikia” Akaendelea kwa kusema:-

Kuhusu kilimo cha miti ninacho kifanya mimi na nimepania kwelikweli ndani ya nchi yangu niipendayo Tanzania ni kwamba, kimepata umaarufu wa ghafla miaka ya hivi karibuni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ongezeko la mahitaji ya mazao ya miti na changamoto ya mazingira. Katika Tanzania mkoa wa Iringa ni moja ya mikoa maarufu inayoongoza kwa misitu mikubwa ya kupandwa. Miti inatumika kwa mbao, nguzo za umeme, nguzo za kujengea pamoja na utengenezeaji wa karatasi.


Ukiacha mahitaji haya tuliyoyazoea; hivi sasa kumeibuka fursa nyingine mpya ambapo mashirika ya kimazingira kutoka Magharibi yananunua hewa ukaa. Kwa maana hiyo unaweza kupanda shamba la miti halafu ukawa unakusanya dola kwa kuuza hewa ukaa wakati ukisubiri miti ikomae uvune mbao, nguzo ama miti ghafi ya kutengenezea karatasi.(Hii ni sawa na kutegeneza hela ukiwa umelala) Mbali na kuuza hewa ukaa, vile vile unaweza kufuga nyuki na kuendelea kuvuna asali wakati unasubiri kukusanya mamilioni kwa kuuza miti ya nguzo, karatasi ama mbao


Kilimo hiki cha miti ni uwekezaji wa muda wa kati na mrefu (middle& long term investments). Kiutamaduni watanzania wengi huwa hawavutiwi na uwekezaji wa muda mrefu. Hata hivyo kama una mpango wa kuwa na “financial freedom” usikwepe kufikiria uwekezaji wa muda mrefu. Waingereza husema “Information is power”. Wengi hawajachangamkia fursa hii kwa kukosa taarifa tu. Kazi yangu leo ni kukupa taarifa hizi za utajirisho.


Miti ya mbao inatumia wastani wa miaka sita hadi 8 au saba, tangu kupandwa hadi kuvunwa kwake. Hii ina maana inapofikisha umri wa miaka sita huwa tayari kwa kuanza kuvunwa kwa mbao ndogo. Ekari moja ya shamba inachukua wastani wa miti mia sita (600). Wastani wa chini wa mti mmoja kwa sasa uliokomaa ni shilingi elfu ishirini (30,000 hadi 60,000,inategemea na ukubwa wa mti). Ina maana katika ekari moja ukiwa na miti iliyokomaa unakusanya jumla ya shilingi milioni kumi na mbili (18,000,000). 
Fedha hiyo (kadirio la chini kabisa) utaipata ikiwa unaamua kuuza kwa bei ya jumla miti ikiwa shambani. Lakini kama ukiamua kupasua mbao wewe mwenyewe unaweza kuvuna mbao hadi za milioni ishirini na tano (32,000,000) kwa ekari moja. Hadi sasa uhitaji(demand) wa mbao katika soko ni mkubwa kuliko ugavi (supply) hivyo kwa miaka 10 ijayo hatutarajii kushuka kwa soko la mbao, nguzo ama malighafi za karatasi.

Gharama ya kununua shamba tupu ni kati ya shilingi  laki moja na 20 elfu (120,000) na laki moja,kutegemea na maeneo husika unayotaka ama kupata. Gharama za kuandaa shamba, kununua miche na kupanda ni kati ya shilingi laki moja  na nusu,na laki moja. Hii ina maana unaweza kumiliki ekari moja ya msitu wa miti kwa hadi shilingi laki sita tu! Kutegemea na umri wa miti unayotaka.

Mtu unaweza kuona kuwa pengine kununua shamba tupu na kuanza kuhangaika na upandaji miti itakuwa ni mlolongo mkubwa; kukusaidia katika hilo nimekuwa na utaratibu wa kumilikisha mashamba yenye miti (kuuza) kwa bei nafuu sana. Yapo mashamba yenye miti ya kuanzia mwaka mmoja, miaka miwili, miaka mitatu na miaka minne. Uponunua mashamba haya kutoka kwangu, mimi naendelea na upandaji wa mashamba mapya kupitia fedha hizo.

Kilimo cha miti ni rahisi sana kwa sababu ukishapanda hakihitaji uangalizi mkubwa sana na wala hauhitajiki uwe karibu na shamba/mradi muda wote. Kuna kazi chache ambazo zinahitajika ukishapanda shamba lako. Mvua inyeshe ama isinyeshe mti wa mbao, nguzo ama karatasi ukishachipua huwa haufi kwani huendelea kutumia unyevu wa ardhini.

Kazi namba moja unapokuwa umeshakamilisha upandaji wa miti kwenye shamba; ni kutengeneza njia za kuzuia moto walau mara moja kwa mwaka, kazi ya pili ni kufyekea miti inapokua walau kwa mwaka mara moja (prooning). Gharama zote hizo yaani kutengeneza njia za moto, kufyekea na kulinda moto haizidi laki mbili kwa mwaka mzima.

Kwa maana hii gharama za kuhudumia shamba la miti ekari moja kutoka kupandwa hadi kuvunwa ni wastani wa shilingi milioni moja tu. Gharama hizi ninazopiga ni ikiwa utaamua kununua shamba leo na kama ungekuwa tayari una shamba ambalo unalihudumia leo.

Hata hivyo nadhani wote tunafahamu kuwa ardhi ni rasilimali inayopanda thamani kila siku. Vile vile tunatambua kuwa suala la mazingira ni tete kwa sasa na katika karne zijazo kama wataalamu wanavyotuthibitishia. Hii ina maana kuwa ukiwa na shamba la miti leo; thamani ya ardhi hiyo inazidi kupanda kila siku na miti uliyopanda inazidi kupanda thamani kila kukicha.

Jambo la uhakika ni kuwa hata kama bei ya miti, mbao, nguzo itayumba hutaweza kupoteza mtaji uliotumia na wala hutakosa kuzalisha faida kwa shamba utakalokuwa umemiliki, iwe ni eka moja, kumi, mia ama elfu moja. Mbali na hivyo unaweza ukaona, ahaa, miaka sita hadi kumi ni mingi mno; bado una nafasiya kupata faida hata ndani ya mwaka mmoja, miwili n.k.

Ukishapanda shamba la miti ekari moja kisha baada ya mwaka mmoja ukaamua uuze utauza si chini ya milioni mbili hadi nne. Kukusanya milioni nne kwa mtaji wa laki sita, pasipo kutumia muda mwingi ama usumbufu wa kusimamia; hakika ni faida nono.

Huenda hadi kufika hapa unaweza ukawa umeshavutiwa na biashara hii. Wengi wenu mnaweza kujiuliza maswali mkubwa mawili; “Ninatamani nifanye mradi huu lakini Iringa sikufahamu na hata kama nakufahamu nitaanzia wapi kupata hayo maeneo?” Pili: Niko mbali na sina muda wa kushinda Iringa, Je, ni nani atanisaidia kupanda, kusimamia na kuendesha hayo mashamba?

Ili kutimiza ndoto yangu hiyo nimeweka utaratibu ufuatao utakaohakikisha kila mwenye ndoto, kiu na hamasiko la kuwekeza kwenye kilimo cha miti anafanikiwa.  Jisikie huru wakati wowote kuwasiliana nami kwa ufafanuzi na msaada wa fursa hii. Natamani watanzania tuache kulalamika kuhusu wageni kuvamia ardhi yetu, badala yake tuchangamke kumiliki na kufanya uzalishaji katika ardhi yetu. Inawezekana!

Kwa kutumia sheria ya ardhi ya mwaka 1999 sheria namba 5 utapata documents za umiliki; kwa kuzingatia taratibu na tamaduni zote za wenyeji zinazohusiana na umilikaji ardhi nitahakikisha nakusaidia ili ndoto yako itimie.

Yupo Baba yangu anaishi Mafinga ambae siku za karibuni amepewa Tuzo ya Rais kwa kuwa mpandaji namba moja wa miti na utunzaji wa mazingira,ameahidi kutoa msaada kwa Mtanzania wa ndani na nje ya Tanzania kumsadia kupata eneo la kupanda miti na kauli ya siku zote ni “USIKUBALI KUWA MNYONGE WA KIUCHUMI NDANI YA TANZANIA.

meshackmaganga@gmail.com

Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/05/usikubali-kuwa-mnyonge-wa-kiuchumi-ndani-ya-tanzania-meshack-maganga.html#ixzz2TpPAljvU

13 Mar 2013

USIYOYAJUA KUHUSU KILIMO CHA MITI

Picha na Maelezo kutoka Mjengwablog
Imeandikwa na Albert Sanga, Iringa

Miezi kadhaa iliyopita kupitia Redio TBC Taifa, ofisa mmoja wa Wizara ya Maliasili na Utalii aliulizwa swali hili, "Je, inawezekana watu binafsi kufungua mashamba ya miti na kufanya biashara ya kuuza miti ya mbao?" Ofisa huyo alijibu hivi, "...inaruhusiwa...hata mimi najilaumu kuwa miaka ile wakati tunapanda msitu wa serikali kule Mufindi mimi sikukumbuka kutafuta maeneo kwa wenyeji nikapanda miti. Kama ningefanya hivyo nadhani leo na mimi ningekuwa milionea". Mahojiano yale yamenipa hamasa ya kuileta makala hii wiki hii.
 
Tangu mwanzoni mwa mwaka huu nimekuwa nikiandika makala za hamasa na ujenzi wa fikra kuhusu mitazamo yetu na uthubutu wa kufanikiwa kupitia biashara. Nikiamini kuwa wengi mmeshajenga mitazamo chanya na utayari kuhusu biashara na uwekezaji, sasa nachukua hatua mpya.
Hatua hii ni ya kuonyesha na kuchambua tija (pay offs) za fursa mbalimbali za kibiashara. Hadi kufika mwishoni mwa mwaka huu nimepanga kuwashirikisha fursa takribani kumi pamoja na utaratibu maalumu wa kuwasaidia wote watakaohitaji kuzichangamkia fursa hizo. Fursa nayoanza nayo leo ni hii ya kilimo cha miti.
Nitakueleza kila kitu ikiwamo, hali ya biashara hiyo kwa sasa na miaka ijayo, gharama na hatua za kuanzisha biashara hiyo, na usimamizi wa biashara hii. Na mwisho kabisa nitakueleza jinsi nilivyojipanga kukusaidia wewe utimize ndoto yako ya kumiliki mashamba ya miti ikiwa utahitaji kufanya hivyo.

Kilimo cha miti kimepata umaarufu wa ghafla miaka ya hivi karibuni kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo ya ongezeko la mahitaji ya mazao ya miti na changamoto ya mazingira. Katika Tanzania, Mkoa wa Iringa ni moja ya mikoa maarufu inayoongoza kwa misitu mikubwa ya kupandwa. Miti inatumika kwa mbao, nguzo za umeme, nguzo za kujengea nyumba na utengenezeaji wa karatasi.
Ukiacha mahitaji haya tuliyoyazoea hivi sasa kumeibuka fursa nyingine mpya ambako mashirika ya kimazingira kutoka Magharibi yananunua hewa ukaa (carbon dioxide). Kwa maana hiyo unaweza kupanda shamba la miti halafu ukawa unakusanya dola kwa kuuza hewa ukaa wakati ukisubiri miti ikomae uvune mbao, nguzo au miti ghafi ya kutengenezea karatasi.

Binafsi niliichangamkia biashara hii miaka minne iliyopita na 'I'm real serious with it'. Nimejiwekea lengo la kupanda ekari 20 kila mwaka. Kilimo hiki cha miti ni uwekezaji wa muda wa kati na mrefu (middle & long term investments). Kiutamaduni Watanzania wengi huwa hawavutiwi na uwekezaji wa muda mrefu.
Hata hivyo, kama una mpango wa kuwa na baadaye imara kiuchumi usikwepe kufikiria uwekezaji wa muda mrefu. Waingereza husema "Information is power". Wengi hawajachangamkia fursa hii kwa kukosa taarifa tu.

 Kazi yangu leo ni kukupa taarifa hizi za utajirisho.

Ekari moja ya shamba inachukua wastani wa miti 600. Wastani wa chini wa mti mmoja kwa sasa uliokomaa ni Sh 20,000. Ina maana katika ekari moja ukiwa na miti iliyokomaa unakusanya Sh milioni 12. Fedha hiyo (kadirio la chini kabisa) utaipata ikiwa unaamua kuuza kwa bei ya jumla miti ikiwa shambani. Lakini kama ukiamua kupasua mbao wewe mwenyewe unaweza kuvuna mbao hadi za 25,000,000 kwa ekari moja.
Gharama ya kununua shamba tupu ni kati ya Sh 200,000 hadi Sh milioni moja kutegemea na maeneo husika unayotaka au kupata. Gharama za kuandaa shamba, kununua miche na kupanda ni kati ya Sh 400,000 hadi Sh 600,000. Hii ina maana unaweza kumiliki ekari moja ya msitu wa miti kwa hadi Sh 600,000 tu.

Kilimo cha miti ni rahisi sana kwa sababu ukishapanda hakihitaji uangalizi mkubwa sana na wala hauhitajiki uwe karibu na shamba/mradi muda wote. Kuna kazi chache ambazo zinahitajika ukishapanda shamba lako. Mvua inyeshe au isinyeshe mti wa mbao, nguzo au karatasi ukishachipua huwa haufi kwani huendelea kutumia unyevu wa ardhini. Kazi namba moja unapokuwa umeshakamilisha upandaji wa miti kwenye shamba, ni kutengeneza njia za kuzuia moto walau mara moja kwa mwaka. Kazi ya pili ni kufyekea miti inapokua walau kwa mwaka mara moja. Gharama zote hizo, yaani kutengeneza njia za moto, kufyekea na kulinda moto haizidi Sh 200,000 kwa mwaka mzima.
 
Miti hukomaa kuanzia miaka sita hadi 10 kutegemea na utunzaji unaoufanya. Hii ina maana kuwa ukichukua Sh 200,000 unazogharimia shamba kila mwaka ukazidisha mara sita unapata Sh 1,200,000.
Kwa maana hii gharama za kuhudumia shamba la miti ekari moja kutoka kupandwa hadi kuvunwa ni kati ya Sh milioni 1.2 hadi Sh milioni mbili. Ukichanganya na gharama ya kupata ardhi na kupanda miti yenyewe unapata kuwa gharama nzima hadi unavuna ni kati ya Sh 2,000,000 kwa kadirio la chini.
Hapa ili kuokoa nafasi nimeweka makadirio yaliyochanganya milinganyo ya muda wa kuvuna, eneo unalopata pamoja na thamani ya fedha katika muda husika. Gharama hizi ninazopiga ni ikiwa utaamua kununua shamba leo na kama ungekuwa tayari una shamba ambalo unalihudumia leo.

Hata hivyo, nadhani wote tunafahamu kuwa ardhi ni rasilimali inayopanda thamani kila siku. Vile vile tunatambua kuwa suala la mazingira ni tete kwa sasa na katika karne zijazo kama wataalamu wanavyotuthibitishia. Hii ina maana kuwa ukiwa na shamba la miti leo, thamani ya ardhi hiyo inazidi kupanda kila siku na miti uliyopanda inazidi kupanda thamani kila kukicha.
Jambo la uhakika ni kuwa hata kama bei ya miti, mbao, nguzo itayumba hutaweza kupoteza mtaji uliotumia na wala hutakosa kuzalisha faida kwa shamba utakalokuwa umemiliki, iwe ni eka moja, kumi, mia au elfu moja. Mbali na hivyo unaweza ukaona, ahaa, miaka sita hadi 10 ni mingi mno; bado una nafasi ya kupata faida hata ndani ya mwaka mmoja, miwili na kadhalika.
Ukishapanda shamba la miti ekari moja kisha baada ya mwaka mmoja ukaamua uuze utauza si chini ya milioni mbili hadi nne. Kukusanya milioni nne kwa mtaji wa laki sita, pasipo kutumia muda mrefu au usumbufu wa kusimamia, hakika ni faida nono.

Huenda hadi kufika hapa unaweza ukawa umeshavutiwa na biashara hii. Wengi wenu mnaweza kujiuliza maswali makubwa mawili; "Ninatamani nifanye mradi huu, lakini Iringa sikufahamu na hata kama nakufahamu nitaanzia wapi kupata hayo maeneo?" Pili, "Niko mbali na sina muda wa kushinda Iringa, je, ni nani atanisaidia kupanda, kusimamia na kuendesha hayo mashamba?"
Kama si hayo maswali mawili hapo juu huenda ningekuwa nilishaandika makala hii tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Lakini nilisita kuandika fursa hii mapema pasipo kuwa na majibu ya maswali hayo kwa wasomaji. Leo nina majibu hayo. Pia nikujulishe kuwa msimu wa kutafuta na kuandaa mashamba tunaanza Agosti-Oktoba na upandaji ni Novemba-Desemba hadi Januari kwa wanaokuwa wamechelewa.
Sifa kubwa ya ujasiriamali ni kufanya huduma kwa watu wengine, yaani kutafuta mahitaji, shida, matatizo na matamanio yao na kuwatimizia. Kama alivyosema mfanyabiashara mmoja wa Kimarekani, Zig Ziglar; "Utapata unachokitaka ikiwa utawasaidia watu wengine wengi kupata wanachokitaka".
Katika kuwasaidia wengine ili wawekeze katika biashara hii ya mashamba ya miti ninaongozwa na mambo makubwa mawili ninayotaka kuona yakitimia. Mosi, mimi na wewe tuungane na serikali na dunia nzima katika kupambana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kupanda miti mingi.
Pili, nataka nikusaidie wewe ambaye kila siku nimekuhamasisha ufikirie biashara na uwekezaji, uchukue hatua ya kuwekeza ili ujikwamue kiuchumi kwa kuvuna mamilioni. Moja ya ndoto nilizonazo duniani ni kuzalisha na kuendeleza wafanyabiashara na wawekezaji wapya kwa maelfu hadi naingia kaburini. Huo ndiyo wito wangu duniani.

Ili kutimiza ndoto yangu hiyo, nimeweka utaratibu ufuatao utakaohakikisha kila mwenye ndoto, kiu na hamasiko la kuwekeza kwenye kilimo cha miti anafanikiwa. Kupitia mfumo wa biashara zangu nimeanzisha kitengo maalumu kijulikanacho kama Fresh Farms (T).
Kazi yangu kupitia kitengo hiki itakuwa ni kukupa ushauri wa kibiashara, kukutafutia maeneo ndani ya Mkoa wa Iringa kwa ekari unazotaka, kukuandalia hayo mashamba, kukupandia hiyo miti na kusimamia utunzaji wa shamba katika hatua za awali na hata baadaye. Jisikie huru wakati wowote kuwasiliana nami kwa ufafanuzi na msaada wa fursa hii.
Kwa kutumia sheria, taratibu na tamaduni zote za wenyeji zinazohusiana na umilikaji ardhi nitahakikisha nakusaidia ili ndoto yako itimie. Nadhani kwa utaratibu huu ipo siku nami naweza kusimama na kujivunia mazao ya watu waliokombolewa kivitendo kutokana na harakati zangu za kuelimisha watu kuhusu ujasiriamali, uchumi na biashara.
Watanzania tunahitaji ushindi wa kiuchumi kupitia uwekezaji!
stepwiseexpert@gmail.com" stepwiseexpert@gmail.com 0766 742 414/ 0719 127 901
0784286670

17 Feb 2013

UFUGAJI BORA NA RAHISI WA KUKU WA KIENYEJI : Anaandika 'Snochet' -Senior Expert Member wa Jamii Forums

Chanzo cha habari:  Jamii Forums (http://www.jamiiforums.com/ujasiriamali/216290-ufugaji-bora-na-rahisi-wa-kuku-wa-kienyeji-kuku-1-akuzalishie-shilingi-milioni-1-a.html)


Kuna usemi flani unatumiwa na watu wengi sana. unasema; “kazi ndio msingi wa maendeleo ya mtu yeyote” . Hata mimi nakubaliana na usemi huu kwani ni kweli kabisa kazi ndio msingi wa hatua yoyote ya maendeleo ya mtu yeyote chini ya msingi mkuu ambao ni Mungu. Kinyume chake, asiyefanya kazi (ya kuajiriwa/kujiajiri) basi atabaki kuwa maskini na mtu wa shida ya kipato, mahusiano mabaya na wanadamu wenzako, kuwa tegemezi nk. Kwa kuwa tunatamani sana kutoka katika kongwa hili la umasikini wa kipato na hali mbaya ya maisha, tunalazimika kufanya jukumu letu kuu la kumuomba sana Mungu ili atuwezeshe kujua na kufahamu mbinu mbalimbali kisha kujifunza na kufahamu kwa makini tena kwa njia rahisi mno za kututoa katika hali hii ya umaskini uliokithiri.



Ikumbukwe kwamba, kujifunza kwa msisimko tu bila ya kuyaingiza mambo hayo uliyojifunza katika mazoezi na vitendo vya makusudi maishani mwetu ni wazi kwamba hayatatusaidia, bali yatabaki vichwani mwetu kama hadithi tu za alfulelaulela na maisha ya kubahatisha maarufu kamaakadabraakadabra. Hivyo tumuombe sana Mungu wetu ili mafundisho haya yaweze kubadili maisha yetu kwa uchumi bora na endelevu ili tuweze kupata kipato na kurudishia Mungu zaka na sadaka badala ya kukaa kulalamika kuwa hatuna cha mkurudishia muumba wetu YEHOVA.


Kama ilivyo chumvi ya dunia, ufugaji pia huhitaji upendo, uvumilivu, karama, utu na maombi ya dhati ambayo yatazaa namna nzuri ya kuipenda kwa dhati ya moyo wako kazi hii ya ufugaji. Vinginevyo utabakia kuwa mtu wa kujaribu na kuishia kushindwa kila mara. Kama ilivyo kanuni ya maendeleo yoyote yale, ufugaji wa kuku pia huhitaji; Ubunifu, utundu wa akili, kujaribu bila kukata tamaa, kugundua, kujifunza, kufanyia kazi mawazo yaa wengine, kusoma vitabu na majarida mbalimbali yahusuyo kazi yako, kujishughulisha nk. Hata ukifundishwa darasani huwezi kufundishwa vyote na mwalimu wako, vingine itakubidi utafute mahali pengine kwa ubunifu mkubwa, ugunduzi na mambo mengine mengi ili ufanikishe lengo la kupata elimu bora ya kile unachokitaka. Hii huhusisha akili yako vema katika kujifunza kutoka kwa watu au vitu vingine nk. Lakini mafanikio zaidi yatapatikana pale utakapokuwa katika utendaji zaidi.

UFUGAJI WA KUKU WATANO (5) WA KIENYEJI UPATE KUKU MIA MBILI (200) KWA MIEZI SITA (6) TU!
(Kuku 200 x 5,000 = 1,000,000)
Unaweza ukaniona kama mimi ni kichaa na ninaye ota ndoto za mchana ambazo hazina mafanikio wala tija maana nadharia hii inaweza isiwaingie vizuri watu vichwani mwao. Watu wengi wamekuwa wakisema na kushauri hata kushauriwa hata na wale wasiofaa. Ninaamini wengi wetu hawapendi kuamini kile wanachoambiwa hadi pale watakapoona kwa macho yao ndipo waamini (akina Tomaso). Sikia nikuambie! kama huamini haraka kitu chochote hebu usimkatishe tamaa yule aliyekwambia habari hizo za kukatisha tamaa, badala yake jaribu kupeleleza na kufuatatilia hatua kwa hatua tena kwa makini maelezo uliyopewa, kisha yaweke katika utendaji (tenda/fanya) kwa ufanisi kisha subiri matokeo. Baada ya kupata matokeo sasa unaweza kwenda mbele kidogo ukauliza/kusoma/kujifunza zaidi ili kuona kama kuna mahali umekosea au hukuzingatia kanuni na maelekezo uliyopewa. Baada ya kupata maelezo ya ziada hebu rudia kufanya tena kwa kuboresha kupitia maelekezo ya awali na hayo mapya uliyopata yote kwa pamoja ili upime matokeo yake. Hapo sasa utakuwa upo kwenye haki ya kuamini au kutoamini kwamba jambo hilo ni kweli au siyo kweli na siyo kutaa tu kwa ubishi usiokuwa na maana yeyote. Kwa kufanya hivi hakika utapiga hatua mbele katika kuboresha maisha yako ya sasa na ya baadae. Ila ukifanikiwa usije ukamkufuru Mungu aliyekuwezesha.



Hebu anza na kuku Watano (5) tu Majike wenye Rika/Umri mmoja (au wanaokaribiana). Watunze vizuri kwa kuwapatia chakula kilicho na mchanganyiko kamili wa viini lishe vinavyotakiwa katika mwili wa kuku, yaani; wanga, protini, calcium, chumvichumvi, madini joto nk(kama nilivyoeleza hapa chini). Wawekee na Jogoo mmoja mzuri wa kienyeji/kizungu/chotara (kama nilivyoeleza hapa chini juu ya uchaguzi wa majogoo).
Wanapoanza kutaga watayarishie mahali pazuri/Kiota kizuri cha kutagia na kuatamia kwa kuwajengea viota ndani ya banda. Hakikisha mahali hapo hapavuji wala hapapati unyevunyevu wala joto kali sana. Hakikisha mahali hapo pana usalama wa kutosha (mahali wanyama hatari kama vicheche, pakashume, nyoka nk hawawezi kufika).
Kuku wakiendelea kutaga na sasa ukaona wanakaribia kuatamia,Anza kuchagua aina ya mayai unayotaka kuku wako walalie. Hii inamaanisha kuwa; ukichagua mayai makubwamakubwa hayo yanakuwa na vifaranga majogoo na mayai madogomadogo mara nyingi huwa ni ya vifaranga majike. Acha kuwawekea mayai ya mviringo kama mpira!
Hakikisha kuku wote wanasubiriana ili walalie/waatamie kwa pamoja.
Weka mayai 12 hadi 15 kwa kila kiota cha kuku 1 kulingana na umbo la kuku wako. Kuku anaweza kutaga hadi mayai 30 kwa kila msimu wa kutaga unapofika. Unaweza kutumia mayai machache kati ya 30 kwa kumuatamishia kuku wako huku mayai mengine yakisubiri awamu ya pili ya kuatamiwa.Kwa mfano ukiwawekea kuku wako hao watano, Kuku 5 x Mayai 12 = Mayai 60.

Kwa kawaida kuku huatamia/hulalia mayai kwa siku 19 hadi 21/24 tu hadi anapototoa vifaranga. Hakikisha unawawekea kuku walioatamia chakula chenye viini lishe vya kutosha na maji mengi karibu na viota vyao ili wakitoka kwenye viota vyao wale chakula mara moja na kunywa maji kisha warudi haraka kwenye mayai yao. Hii itasaidia kuangua mayai yote 12/15 bila kuharibu yai hata moja. Au hata yakiharikbika basi hayataharibika mengi kama ukiacha kuwawekea chakula waende kufukuzana na panzi na vyakula majalalani huko nje na kuchelewa kurudi kwenye mayai yao.

15 Feb 2013

NAMNA YA KUBORESHA UFUGAJI WA KUKU - MAKALA YA 'MKULIMA MBUNIFU'

Ufugaji wa kuku wa kienyeji unaweza kuimarika kupitia uzalishaji na utunzaji sahihi
Wafugaji wengi wa Tanzania wanafuga kuku wa kienyeji. Ndege hawa kwa kawaida wanafugwa sehemu za vijijini ambapo wanaachiwa huru kuzurura.


Kuna uwezekano mkubwa sana wa kizazi kujirudia kwa kuwa jogoo anaweza kumpanda mtetea ambaye alitokana naye, au kumpanda mtetea ambaye wamezaliwa pamoja. Kuzaliana kwa namna hiyo kunasababisha matatizo makubwa, ikiwa ni pamoja na kudumaa, kupunguza uzalishaji wa mayai, kuwa na vifaranga dhaifu ambavyo ni rahisi kushambuliwa na magonjwa, na mengineyo mengi yasiyokuwa ya kawaida. Ufugaji huru ambao una udhibiti ni muhimu sana ili kuepuka kizazi kujirudia. Kuku wanaweza kuwekwa kwenye makundi na kuachiwa kwa makundi ili kuzuia uwezekano wa kuzaliana kwa kizazi kimoja.

Mfugaji anayetaka kufanikiwa katika ufugaji wa kuku wa kienyeji ni lazima achanganye mbinu za kienyeji na za kisasa. Hii inajumuisha njia zifuatazo:

Kuchagua aina/mbegu 
Kuchagua mbegu inamaanisha: Mtetea au jogoo mwenye ubora wa hali ya juu , akiwa na sifa kama uzalishaji wa juu wa mayai au uzalishaji wa nyama, wanachanganywa na aina mfugaji alionayo, au kuboresha mbegu ambayo ni dhaifu. Kuna makundi matatu ya aina za kuku;

• Kuku wenye umbo dogo ni wazuri zaidi kwa uzalishaji wa mayai.
• Kuku wenye umbo kubwa ni wazuri zaidi kwa uzalishaji wa nyama.
• Mbegu iliyochanganywa ni nzuri kwa uzalishaji wa mayai na nyama.

Endapo mfugaji anataka kufuga kuku kwa ajili ya mayai, basi anaweza kuchanganya mbegu ya kienyeji aliyonayo na mbegu yenye umbo dogo ambao wana historia nzuri ya uzalishaji wa mayai, na kama anataka kuzalisha kwa ajili ya nyama, basi anaweza kuchagua wenye umbo kubwa. Na ambae anahitaji kwa ajili ya mayai na nyama, basi anaweza kuchanganya mbegu.
 
Chagua mbegu kwa umakini
Wafugaji wenye uzoefu huchanganya mbegu tofauti ambazo zina ubora na sifa maalumu, kama vile uwezo wa kukabiliana na magonjwa, ukubwa wa mayai, umbo, na kiasi cha chakula wanachohitaji.

Vigezo vifuatavyo vinaruhusu uchaguzi sahihi:
1. Mtetea au jogoo kati ya kilo 1 mpaka 2, anahesabiwa kuwa kwenye kundi la umbo dogo.
2. Kuku wote wenye uzito wa kilo 3 au zaidi wanahesabiwa kwenye umbo kubwa.
 
Kuku wenye kilo 2 mpaka 3 wanahesabiwa kuwa mbegu mchanganyiko (Chotara). Uzalishaji mzuri wa kuku ni pamoja na kuhakikisha kuwa, kila baada ya mzunguko mmoja, jogoo anabadilishwa, au kuku wote pamoja na mayai yake wanauzwa na kuleta aina nyingine ili kuzuia kizazi kujirudia. Ruhusu jogoo mmoja kuhudumia kuku 10 tu. Mfugaji pia anaweza kuzuia uwezekano wa kizazi kujirudia kwa kuweka kumbukumbu rahisi, kwa mfano, unaweza kuweka viota na kufahamu ni kuku yupi yupo kwenye kiota kipi na kwa muda upi.

Kumbukumbu ni muhimu  
Uwekaji wa kumbukumbu ni lazima! Kumbukumbu humsaidia mfugaji kufahamu kizazi na tabia za kila kuku ambaye amechaguliwa kwa ajili ya uzalishaji, kiasi kwamba anaweza kuelezea kuhusu kila kuku aliye naye bandani, kwa kuzingatia uzalishaji wa mayai na nyama.

CHANZO (Source): http://www.mkulimambunifu.org