Our Activities and Projects/Shuguli na Miradi ya UDT

Uwanji Development Trust (U.D.T) is a charitable, non-profit making, community-based trust. UDT was established in 2008 and became registered on 28th July 2010 by a certificate of registration no.S.A.16950 under society ordinance act 1954, society Act cap 337 (R.E.2002) of the United Republic of Tanzania. UDT is involved with several activities which include, but are not limited to, the following; 1.Promoting access and provision of quality education; 2. Provide assistance on health matters with special focus on HIV/AIDS; 3.Take measurable actions on the protection of environment; 4. Cooperate with governmental and non governmental stakeholders for technical and financial sustainable development issues and act as implementing agency; 5. Perform any other activity for the sustainable development of Uwanji people.
Join our cause by writing us: Our email address is udt2010[at]live.com or contact one of the following for more details; Chaiperson -Toba Nguvila - +255 755 097181. Deputy Chairperson - Rev. Naibu Nyambo +255 754 387364. Secretary - Valentine Malila - +255 755 474579. Deputy Secretary - Amani Mbwilo - +255 753 858527.

15 Feb 2013

NAMNA YA KUBORESHA UFUGAJI WA KUKU - MAKALA YA 'MKULIMA MBUNIFU'

Ufugaji wa kuku wa kienyeji unaweza kuimarika kupitia uzalishaji na utunzaji sahihi
Wafugaji wengi wa Tanzania wanafuga kuku wa kienyeji. Ndege hawa kwa kawaida wanafugwa sehemu za vijijini ambapo wanaachiwa huru kuzurura.


Kuna uwezekano mkubwa sana wa kizazi kujirudia kwa kuwa jogoo anaweza kumpanda mtetea ambaye alitokana naye, au kumpanda mtetea ambaye wamezaliwa pamoja. Kuzaliana kwa namna hiyo kunasababisha matatizo makubwa, ikiwa ni pamoja na kudumaa, kupunguza uzalishaji wa mayai, kuwa na vifaranga dhaifu ambavyo ni rahisi kushambuliwa na magonjwa, na mengineyo mengi yasiyokuwa ya kawaida. Ufugaji huru ambao una udhibiti ni muhimu sana ili kuepuka kizazi kujirudia. Kuku wanaweza kuwekwa kwenye makundi na kuachiwa kwa makundi ili kuzuia uwezekano wa kuzaliana kwa kizazi kimoja.

Mfugaji anayetaka kufanikiwa katika ufugaji wa kuku wa kienyeji ni lazima achanganye mbinu za kienyeji na za kisasa. Hii inajumuisha njia zifuatazo:

Kuchagua aina/mbegu 
Kuchagua mbegu inamaanisha: Mtetea au jogoo mwenye ubora wa hali ya juu , akiwa na sifa kama uzalishaji wa juu wa mayai au uzalishaji wa nyama, wanachanganywa na aina mfugaji alionayo, au kuboresha mbegu ambayo ni dhaifu. Kuna makundi matatu ya aina za kuku;

• Kuku wenye umbo dogo ni wazuri zaidi kwa uzalishaji wa mayai.
• Kuku wenye umbo kubwa ni wazuri zaidi kwa uzalishaji wa nyama.
• Mbegu iliyochanganywa ni nzuri kwa uzalishaji wa mayai na nyama.

Endapo mfugaji anataka kufuga kuku kwa ajili ya mayai, basi anaweza kuchanganya mbegu ya kienyeji aliyonayo na mbegu yenye umbo dogo ambao wana historia nzuri ya uzalishaji wa mayai, na kama anataka kuzalisha kwa ajili ya nyama, basi anaweza kuchagua wenye umbo kubwa. Na ambae anahitaji kwa ajili ya mayai na nyama, basi anaweza kuchanganya mbegu.
 
Chagua mbegu kwa umakini
Wafugaji wenye uzoefu huchanganya mbegu tofauti ambazo zina ubora na sifa maalumu, kama vile uwezo wa kukabiliana na magonjwa, ukubwa wa mayai, umbo, na kiasi cha chakula wanachohitaji.

Vigezo vifuatavyo vinaruhusu uchaguzi sahihi:
1. Mtetea au jogoo kati ya kilo 1 mpaka 2, anahesabiwa kuwa kwenye kundi la umbo dogo.
2. Kuku wote wenye uzito wa kilo 3 au zaidi wanahesabiwa kwenye umbo kubwa.
 
Kuku wenye kilo 2 mpaka 3 wanahesabiwa kuwa mbegu mchanganyiko (Chotara). Uzalishaji mzuri wa kuku ni pamoja na kuhakikisha kuwa, kila baada ya mzunguko mmoja, jogoo anabadilishwa, au kuku wote pamoja na mayai yake wanauzwa na kuleta aina nyingine ili kuzuia kizazi kujirudia. Ruhusu jogoo mmoja kuhudumia kuku 10 tu. Mfugaji pia anaweza kuzuia uwezekano wa kizazi kujirudia kwa kuweka kumbukumbu rahisi, kwa mfano, unaweza kuweka viota na kufahamu ni kuku yupi yupo kwenye kiota kipi na kwa muda upi.

Kumbukumbu ni muhimu  
Uwekaji wa kumbukumbu ni lazima! Kumbukumbu humsaidia mfugaji kufahamu kizazi na tabia za kila kuku ambaye amechaguliwa kwa ajili ya uzalishaji, kiasi kwamba anaweza kuelezea kuhusu kila kuku aliye naye bandani, kwa kuzingatia uzalishaji wa mayai na nyama.

CHANZO (Source): http://www.mkulimambunifu.org

No comments: