Hello wanaUDT,
Mghonile!
Unenilinkafu.
Kama ambavyo unaona, hili cha chapisho la kwanza la majaribio kwenye ukurasa-mtandao (webpage) wa UDT. Kama ukurasa mtandao utapata kura za kutosha basi unaweza kuendelezwa ama lasivyo tukatafuta njia nyingine.
Tafadhali tupia macho kwenye anuani ya ukurasa mtandao (www.uwanjikwanza.blogspot.com) na angalia kama jina la uwanjikwanza linafaa kwani kuna uwezekano wa kubadilisha. Tukitaka kuondokana na neno blogspot na kuwa na kitu kama www.uwanjikwanza.org inatupasa kulipia dola kumi kwa mwaka, ni rahisi na inawezekana.
Sijaona kauli mbiu ya UDT kwenye katiba (kama ipo naomba kufahamishwa). Tupia macho kwenye kauli mbiu ya UDT isiyorasmi inayoonekana kwenye ukurasa-mtandao huu yaani - LENGO NI MAENDELEO, NJIA NI USHIRIKIANO (THE GOAL IS DEVELOPMENT and THE METHOD IS COOPERATION) na toa maoni yako kwenye comments hapo chini.
Pamoja daima
Joshua Mhalila
No comments:
Post a Comment