Our Activities and Projects/Shuguli na Miradi ya UDT

Uwanji Development Trust (U.D.T) is a charitable, non-profit making, community-based trust. UDT was established in 2008 and became registered on 28th July 2010 by a certificate of registration no.S.A.16950 under society ordinance act 1954, society Act cap 337 (R.E.2002) of the United Republic of Tanzania. UDT is involved with several activities which include, but are not limited to, the following; 1.Promoting access and provision of quality education; 2. Provide assistance on health matters with special focus on HIV/AIDS; 3.Take measurable actions on the protection of environment; 4. Cooperate with governmental and non governmental stakeholders for technical and financial sustainable development issues and act as implementing agency; 5. Perform any other activity for the sustainable development of Uwanji people.
Join our cause by writing us: Our email address is udt2010[at]live.com or contact one of the following for more details; Chaiperson -Toba Nguvila - +255 755 097181. Deputy Chairperson - Rev. Naibu Nyambo +255 754 387364. Secretary - Valentine Malila - +255 755 474579. Deputy Secretary - Amani Mbwilo - +255 753 858527.

20 Aug 2013

NDEGE AITWAYE KWALE AWEZA KUWA CHANZO CHA KIPATO CHA UHAKIKA!

[Habari hii imenukuliwa kutoka www.wavuti.com]

Kuna wakati nilijiamini kuwa ninakifahamu vilivyo Kiswahili. Lakini kadiri siku zinavyokwenda, ndiyo ninavyozidi kugundua kuwa nina uhaba wa misamiati ya lugha yangu Mama.

Kwa mfano, kwetu tukiwa watoto tulikuwa tukimwinda ndege/kuku huyu nyakati za masika na tulimtambua kwa jina la 'kware,' sikufahamu kuwa jina lake jingine ni 'tombo' mpaka nilipoisoma habari ifuatayo...
Picture
Madai kwamba ulaji wa bidhaa za tombo husaidia afya ya mtu ni sehemu ya sababu ya hivi karibuni ya kuongezeka kwa mahitaji nchini Kenya. [Bosire Boniface/Sabahi]
Kutokana na hali ya wimbi kubwa la mahitaji ya bidhaa za tombo katika miezi ya hivi karibuni kumelazimisha wafanyabiashara nchini Kenya kote kujiingiza katika biashara mpya ya ufugaji wa tombo.

Mkaazi wa Kiambu Andrew Githinji aliiambia Sabahi kwamba ufugaji wa tombo hauna gharama kuendesha na unaleta mapato mazuri: "Hauhitaji eneo kubwa. Tofauti na kuku ambao wanahitaji eneo kubwa, viota vya [tombo] vinaweza kuwekwa vibarazani," Githinji alisema.

Alisema kwa mara ya kwanza alivutiwa na mradi kama huo baada ya kusoma kwenye orodha ya vyakula katika hoteli yenye nyota tano huko Nairobi mwezi Januari 2012.

Alipata kuona kitu ambacho hakuwa anakijua: nyama ya tombo ya kubanika. "Nilifikiri kuwa tombo alikuwa aina ya chakula kinachotoka baharini, katika kuchunguza, nilimuuliza mhudumu na alisema ilikuwa ni ndege," Githinji mwenye umri wa miaka 33 alisema.

Githinji, ambaye pia anafuga sungura, alianza kufanya utafiti kuhusu tombo na kugundua kuwa watu wanamfuga ndege huyo: "Sikuwa najua kuwa ndege huyu, ambao wanapatikana kwa wingi kijijini kwangu, angeweza kufugika," alisema.

Alinunua ndege wake 20 kwa mara ya kwanza kwa shilingi 250 kila mmoja (dola 2.85), Githinji alisema, akiongezea kwamba kwa sasa ana tombo 520: "Cha kusikitisha tu ni kwamba niligundua biashara hii kwa
kuchelewa," alisema Githinji. "Lakini nitwafikia wengine na kwa muda wa miaka miwili nitakuwa na mashine yangu ya kutotolesha itakayosaidia kutotoleshea vifaranga."

Mkaazi wa Mombasa Alex Mureithi, mwenye umri wa miaka 39, alisema alishangazwa kwenda katika shamba la tombo baada ya kutembelea katika duka la jumla mwezi Julai 2012.

Aliona dazeni za "mayai tofauti ya tombo" katika rafu ambalo alidhania ni nakshi ya jiwe la sabuni na kugundua kwamba walikuwa wakiuza kwa shilingi 650 (dola 7.43) ukilinganisha na trei la mayai 30 kwa bei ya shilingi 400 (dola 4.57).

Mureithi kisha alizungumza na meneja wa duka ambaye alimwambia kwamba wafugaji wa tombo hawawezi kutosheleza mahitaji ya soko, ingawa tombo hutaga mayai karibia kila siku: "Nilitambua kuwa yalikuwa ni matembezi yenye faida hivyo nilinunua ndege 10. Sasa ninao 900," Mureithi aliiambia Sabahi. "Sijui nini kitatokea katika ufugajii wa tombo kwa siku zijazo lakini sasa ninavuna faida ya juu kabisa. Anaziuzia hoteli nne huko Mombasa na Nairobi, ambazo zinatoa agizo kwa kila mwezi kwa wafugaji kupata mayai na nyama ya tombo", alisema.

Anatoza mayai yake kwa shilingi hadi 60 (senti 68) kwa kila moja na tombo mzima kwa shilingi 800 (dola 9.14).

Mureithi pia anawafundisha na kuwatembeza wanaotaka kuwa wafugaji wa tombo katika shamba lake kwa kuwatoza shilingi 3,000 (dola 34.3), alisema.

Nzuri kwa afya ya kila mtu? Mahitaji ya mayai na nyama ya tombo yamesababishwa na ripoti ambazo zinaeleza kwamba kula tombo una thamani ya kiafya.

Yunuke Nyanchama, mkaazi wa Kisii mwenye umri wa miaka 67, aliiambia Sabahi kwamba amekuwa akila mayai ya kituitui kwa miaka miwili iliyopita. Alipatikana na kisukari mwaka 2004 na amekuwa akitumia dawa nyingi bila kuwa na mabadiliko mazuri.

Wakati wa ukaguzi wa kawaida mwezi Mei 2011, hata hivyo daktari wake alipendekeza kwamba ajaribu mayai ya tombo:"Nilistaajabishwa na tiba hiyo, lakini baada ya kutumia mayai hayo na nyama ya ndege, kuna mabadiliko makubwa," alisema.

Vincent Juma, daktari wa Hospitali ya Wilaya ya Mbagathi, aliiambia Sabahi kwamba wakati kulikuwa hakuna utafiti kuhusu faida za kitabibu za mayai na nyama ya tombo, watu wengi wamethibitisha kuwa unafuu baada ya kuvitumia: "Miongoni mwa wagonjwa ambao walirekodiwa [ni] wale waliopata unafuu mkubwa [ni] wale waliokuwa wakisumbuliwa na kifua kukuu na vidonda. Mgonjwa wa saratani alisema kwamba maumivu aliyokua nayo yamepungua baada ya kutumia mayai hayo," Juma alisema

Wafugaji wa tombo wanahitaji leseni Kwa sababu tombo wanachukuliwa kama wanyamapori, wafugaji wa tombo kwanza wanahitaji kuomba kibali kutoka katika Huduma za Wanyamapori Kenya (KWS), msemaji wa shirika hilo Paul Udoto aliiambia Sabahi.

Kabla ya huduma hiyo kutoa leseni, viongozi wa KWS wanapaswa kukagua shamba lake kuhakikisha kwamba linakidhi mahitaji kwa ajili ya kufuga tombo, alisema Udoto.

Malipo ya mwaka kwa ajili ya leseni yanagharimu hadi shilingi 2,000 (dola 22.9), alisema, akiongeza kwamba kibali kinaweza kuhuishwa kwa mwaka kulingana na kukamilisha baadhi ya masharti, ikiwa ni pamoja na usafi.

KWS inaendesha ufuatiliaji na ukaguzi wa mashamba kwa vipindi, na hufuta leseni kutoka kwa wafugaji ambao wanakiuka masharti hayo, alisema Udoto

Huduma hiyo ina maombi mengi ya kibali kutoka kwa watu binafsi na vikundi ambavyo vinataka kufanya ufugaji wa tombo, alisema.

Serikali inahamasisha biashara iliyorekebishwa kama njia ya kuanzisha ajira na kuwapa Wakenya mbadala wa vyanzo vya chakula, alisema Udoto, akiongeza kwamba biashara ya tombo imeota mizizi katika mikoa ya Pwani, Mashariki na Kati pamoja na Kaunti ya Nairobi.

KWS pia inatoa leseni za kufuga wanyamapori wengine kama mamba ili kusaidia katika jitihada za utunzaji, alisema. --- Imeandikwa na Bosire Boniface na kuchapishwa kwenye gazeti la gazeti la Sabahi.

No comments: